Naibu waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI David Silinde ametoa siku tatu kupelekewa taarifa za kwanini ujenzi wa madarasa haujakamilika kwa zaidi ya miezi sita ikiwa hela zote zimetolewa toka kupitia mradi wa kulipa kulingana na matokeo (Ep4r).
Silinde ametoa agizo hilo baada ya kutembelea ujenzi wa madarasa wa Shule ya Sekondari Kintunku iliyopo katika Halmashauri ya Manyoni Mkoani Singida na kukuta ujenzi huo unasuasua huku sababu zikitolewa kuwa ujenzi ni kutokukubaliana kati ya kamati ya shule na mkuu wa shule kuchagua nani awe mkandarasi wa ujenzi hali iliyochukua zaidi ya miezi miwili na ukosefu wa maji kwa ajili ya ujenzi.
Naibu Waziri Silinde hakuridhishwa na sababu hizo na amemuagiza Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Manyoni kuandika maelezo ya kwanini wasichukuliwe hatua kwa uzembe waliofanya kukwamisha wanafunzi kuanza kusoma kwa wakati.
Aidha Silinde amevunja Kamati ya Ujenzi wa Shule kwa kushindwa kusimamia ujenzi kukamilika ndani ya miezi mitatu na sasa ni zaidi ya miezi sita ikiwa bado haujakamilika.
Silinde ametoa wiki tatu kwa ujenzi wa madarasa katika shule ya Kintinku uwe imekamilika. « Nautaka uongozi wa Manyoni kuanzia Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kusomamia ipasavyo ujenzi wa madarasa ili wanafunzi waweze kuanza masomo yao kwa wakati.