Club ya Simba SC kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii zimeweka wazi kuhusiana na wachezaji wao wapya Luis Miquissone na Shiza Kichuya kutowatumia hadi sasa.
Simba imeweka wazi kuwa sababu kuu ya kutowatumia wachezaji hao ni kutokana na kuchelewa kufika kwa ITC zao kutoka mashirikisho ya nchi walizokuwa wanacheza.
Miquissone sasa suala lake lipo katika kamati ya hadi za wachezaji za FIFA kwa nini ITC yake haijafika hadi sasa wakati Kichuya ITC yake kutoka Misri alipokuwa anacheza soka ilitoka lakini imezuiliwa tena hivyo Simba SC wanasubiri majibu ya FIFA.