Uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ulikuwa unatajwa kutaka kumfukuza kocha wao muingereza Dylan Kerr kutokana na kutofurahishwa kwa mwenendo wa timu hiyo hususani kupoteza katika michezo miwili dhidi ya Yanga na Tanzania Prisons.
Licha ya kuwa kitaalamu Simba haikuwa imefanya vibaya sana katika mechi zake za Ligi Kuu maamuzi hayo ya kutaka kumfukuza kocha yalikuwa yanawatatiza wengi, baadae stori zikatoka kuwa kuna moja kati ya watu wa benchi la ufundi hupeleka maneno ya kichonganishi kwa viongozi wa ngazi ya juu kuhusu Dylan Kerr.
Zote hizo zilikuwa stori tu zinazoongelewa na watu na vyombo vya habari ila November 3 uongozi wa klabu hiyo kupitia tovuti rasmi na account zake za mitandao ya kijamii zimetoa majibu kuhusiana na mpango wa kumfukuza kocha Dylan Kerr, katika taarifa hiyo ambayo inatajwa kutoka kwa rais wa klabu hiyo Evans Aveva.
“Klabu ya Simba na hususani uongozi wenu mara zote umeheshimu taaluma na kujitahidi kuhakikisha kocha anafanya kazi yake bila kuingiliwa. Tunaelewa wapenzi na wanachama wangependa tushinde mechi zetu zote, hili pia ni tamanio la uongozi wa Simba”
“Lakini kama ambavyo tulisema hapo awali kuwa ligi ya Tanzania bara msimu wa 2015/2016 itakuwa na ushindani mkubwa. Pia ni vizuri kuzingatia kuwa hadi sasa Simba imecheza mechi nyingi nje ya Dar es Salaam ukilinganisha na wapinzani wetu tena kwenye viwanja ambavyo msimu uliyopita tulipata matokeo mabaya.Kwa niaba ya uongozi wa Simba napenda kuwapa taarifa rasmi kuwa uongozi wenu uko nyuma ya kocha Kerr na tunampa sapoti kadiri ya uwezo wetu”
CHANZO CHA HII STORI: simbasports.co.tz
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.