Siku kadhaa zilizopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alitoa maagizo matatu yanayohusu ombaomba wa mabarabarani kuondoka, majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipo kuwa na parking kutafuta parking na wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Makonda alitoa muda wa siku sita ambapo muda huo umetimia leo April 18 2016, kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro ameyazungumza haya kuhusu ombaomba mbele ya waandishi wa habari ………
>>>’ombaomba wengi wameanza kuondoka, lakini sisi kama jeshi na idara zingine leo hatukuanza rasmi kwa sababu unapowakamata hawa ndugu zetu lazima ujue namna ya kuwasafirisha na ni operesheni inayohusu idara nyingi, kimsingi vijana wangu wamepita maeneo mbalimbali wameona wengi wameondoka’:-Kamanda Sirro
>>>’wasije wakafikiria hii ni nguvu ya soda, tunapanga mpango mkakati mzuri kwa wale wachache ambao watakuwa wamebaki’:-Kamanda Sirro
ULIIKOSA YA MKUU WA MKOA DAR ALIPOYATOA HAYA MAAGIZO MATATU? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE