AyoTV

Mambo 7 yaliyozungumzwa na mdogo wa Samuel Sitta leo Tabora

on

Peter Sitta ni mdogo wake Samuel Sitta na kumbukumbu bado anazo kuhusu maongezi yake ya mwisho aliyofanya na Marehemu Samuel Sitta kabla hajasafiri kwenda Ujerumani kwenye matibabu.

  • Sisi katika familia tulizaliwa wawili, huyo Bwana mdogo wa tatu ni kwa upande wa baba mdogo na yeye tunamchukulia ni pamoja kwakuwa tulimtoa kule nyumbani bado mdogo sana.
  • Mama yetu sisi ni Muislamu nashukuru sana katika kumwambia jambo hili la msiba, kitu alichofanya Sitta kimekuja kusaidia sana katika namna Mama alivyolipokea, alimpeleka mama Hija na amekua mshika sala sana na ni kitu ambacho kimemsaidia sana mama katika kupokea msiba wa Mwanae.
  • Maneno ya mwisho aliyoniambia kabla ya kuondoka tarehe 3 kwenda Ujerumani, alikua ananiambia Peter watu wanajifunza kwa vitendo zaidi kuliko kwa maneno utakayowaambia, wewe ndio unanifata mimi na kule nyumbani wewe ndio kiongozi wa familia jaribu kuwa mfano.
  • Kwenye udogo wake Samuel Sitta alipenda sana kujielimisha, alipenda sana kusoma na alikua akinifundisha, vitu vingi alivyokua akipenda ni pamoja na chochote alichokiamini kukitenda kwa haki, uadilifu na weledi mfano Tabora boys alicheza mpira akiwa Golikipa.
  • Mpaka alipokua mkubwa alipenda sana mpira na alipokua mkubwa alikua shabiki wa Simba na hata alishawahi kuipeleka Brazil.
  • Sitta amenifundisha vitu vingi, amefundisha kupenda watu na kuwasaidia… amesaidia watu wengi sana kielimu, kiafya na mengine… amesaidia kupata matibabu watoto walio na vichwa vikubwa ambao wazazi wao walishindwa kuwalipia.
  • Alipenda sana Ibada, alisaidia sana Makanisa na sio tu lile alilokua akisali bali mpaka madhehebu ya Kiislamu, Roman Catholic na mengine mijini na vijijini, unaweza kutazama video yenyewe Peter akiongea kwa kubonyeza play hapa chini

VIDEO: Zitto Kabwe aliposimama kuuga mwili wa Samuel Sitta bungeni tazama katika hii video hapa chini..

Soma na hizi

Tupia Comments