Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wananchi wa Mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya ujambazi, utekaji katika maeneo hayo.
Lugola alisema uhalifu katika mikoa ya mipakani licha ya kuwa imethibitiwa kwa kiasi kikubwa lakini bado baadhi ya mikoa ukiwemo Mkoa wa Katavi, wahalifu utumia njia zisizo rasmi kuingia nchini na kufanya matukio ya uhalifu.
Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi, aliwataka wananchi hao kutoa taarifa kwa vyombo vya dola, kwa watu ambao wanawatilia mashaka ili kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu.
DPP AKITAJA WAJUJUMU UCHUMI WALIOTUBU, WATARUDISHA BILIONI 107