Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeagiza Sukari kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho Mei 11, 2016.
Ametoa kauli hiyo leo mchana Mei 10, 2016 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi wa sukati ambayo imekwishawasili nchini Waziri Mkuu alisema tani 2000 zitapelekwa (Mikoa ya kaskazini), tani 3,000 (Mikoa ya kanda ya ziwa), tani 2,000 (Mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya kanda ya kati).
‘Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu.Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni’– Waziri Mkuu
Amesema anawataka watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache ‘Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwa Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwasababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai’- Waziri Mkuu
Waziri huyo amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabiashara wadogo ili wao wawauzie wananchi kwa bei elekezi ya Sh.1800, pia amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.
‘Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya Sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi utakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo’- Waziri Mkuu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA YA MBUNGE LIJUA LIKALI KUHUSU KAULI YAKE ‘SERIKALI ISIRUHUSU WAFANYABIASHARA WAAGIZE SUKARI NJE’ ITAZAME HAPA