Dr.Wilbrod Slaa leo amezungumza na waandishi wa Habari Dar es salaam na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyomfanya kuwa kimya ndani ya Chama chake cha CHADEMA.
Hapa nimekuwekea maneno aliyokuwa akiyazungumza mbele ya vyombo mbalimbali vya Habari.
WILIBROD SLAA-Katika maisha yangu yote sijawahi kuona waandishi wengi hivi, ni dalili kwamba watu wanakiu ya kujua #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Ningependa nianze kwamba niliamua kufanya kazi hii leo kwa sababu inafika mahali ukweli lazima usemwe-#MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA- Wengi mnafahamu kwamba sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia kile ambacho ninakiamini mimi #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Niseme tu pia sina chuki na mtu yoyote wala kiongozi yoyote wa chama chochote ingawa nimesikia mengi #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WLIBROD SLAA-Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine, kuna mambo ambayo yalinifanya niwe kimya kwa muda #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Niliamua kuachana na siasa baada ya kuona mambo hayaendi sawa kama nilivyotegemea ndani ya chama changu #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Baada ya LOWASSA kutajwa, mpambe wake Askofu GWAJIMA alinipigia simu akiniambia Dodoma mambo yameiva #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Kama utaratibu, LOWASSA baada ya kusema anahama CCM, alipaswa ajisafishe na tuhuma zote alizokuwa nazo #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-LOWASSA hakufanya hivyo, alipaswa kufanya hivyo akiwa peke yake na si viongozi wa chama anachokwenda #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Si kwamba nilikuwa sitaki LOWASSA agombee Urais,nilitaka tupate mgombea mwenye sifa zote zinazotakiwa #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Mimi sikuwa na shida ya kugombea Urais, ningekuwa nataka ningechukua fomu siku ya kwanza walipotangaza #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Wakati hayo yanaendelea nilikuwa nasimamia uteuzi wa viongozi mbalimbali ndani ya CHADEMA #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Sikuambiwa lolote kama LOWASSA ni Asset au liability ndani ya Chama chetu na ndio maana nilikuwa sielewi#MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Niliandika barua ya kujiuzulu lakini Prof SAFARI akaichana, sikukata tamaa nikaandika tena #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Niliandika tena taarifa rasmi kupeleka kwenye chama,hawajui ukitaka kujiuzulu haina hata haja ya kueleza#MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Maneno mengi yalisemwa mara nimefungiwa ndani na mke wangu, mara nitaitisha kikao na waandishi kesho-#MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA- Walisema Dk Slaa analipwa milioni 7 na CHADEMA,napenda kusema familia yangu inaishi maisha ya kawaida #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Mimi na SUMAYE tunagombana kila siku kwa kuchukua shamba kubwa pale Kibaigwa, alafu leo anajiita msafi #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Niliahidi mwaka huu CHADEMA hatuchukui Makapi, lakini naona wote waliokuja ni mizigo, nawajua A mpaka Z #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA- Ndio maana mpaka leo viongozi wangu wamebaki vigugumizi ndio maana mpaka leo hawawezi kusema lolote #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Leo LOWASSA anasimama jukwaani na kusema leteni ushahidi wa ufisadi hata bado hajapewa kadi ya chama #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘CCM wamekuwa waoga kutoa ushahidi wa mafisadi, na hata LOWASSA alipofikia ni CCM imemlea #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Mwaka 2008 Nilikuwa bungeni kuzungumzia Richmond, tuliyajadili Bungeni wote,hatukuyasoma magazetini #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Mimi ninamlaumu LOWASSA kwa mambo mengi sana na si kashfa ya Richmond pekee kama watu wanavyofikiria #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-Mimi nimeletewa rushwa hadharani asubuhi, nikamwambia kama unanipa milioni 500 nyingine unazitoa wapi? #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Milioni 500 ni nyingi sana, Rushwa ni kitu kinachoanzia kichwani na si katika mazingira ya kawaida #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILIBROD SLAA-‘Mnaweza kusema kwa nini namsema LOWASSA tu, mkumbuke anagombea Urais wa nchi, ukweli hawezi kuvumilika #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILIBROD SLAA-‘Nilimwambia LOWASSA wewe na wenzako ni mafisadi kichwani, kwenye nafsi na moyoni alafu nikakimbia #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-Nimemsikia MWAKYEMBE na SITTA wanamuomba LOWASSA kwenye mjadala ili aweze kueleza mambo yake, safii #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-Nimemsikia MWAKYEMBE na SITTA wanamuomba LOWASSA kwenye mjadala ili aweze kueleza mambo yake, safii #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILBROD SLAA-‘Naumia sana kuona CHADEMA yangu niliyotoka nayo mbali na kufika hapa leo inafikia hatua haiaminiki tena #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
WILBROD SLAA-Sehemu kubwa ya hotuba ya Jangwani ni ilani yetu ambayo tulishaandika toka zamani,LOWASSA hakuweka kipya #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILIBROD SLAA-‘LOWASSA achunguzwe zaidi ya milioni 400 alizopeleka Marekani, wanaomtetea watoke hadharani wakitaka #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Vijana wengi wakisikia CHADEMA wanashawishika, lakini napenda kuwaambia baadaye tusije kulaumiana #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-Mimi huwa naongea kwa kujiamini sana, na siwezi kwenda kushtaki mahakamani, anayetaka kwenda aende #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Mimi sitaki kuingilia sana mambo ya Kina Babu Seya lakini naomba wanasheria wetu wajitokeze kusema #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILIBROD SLAA-‘Akili ya LOWASSA ipimwe,kesi ya ulawiti Rais hapaswi kuingilia, anaingilia uhuru wa mahakama #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA- Afadhali kutokuwa na Rais kama huyo,ni Rais balaa ambaye hawezi kuthamini maisha ya Watanzania #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Akiwa Waziri mkuu alibadilisha hata mpaka wa Monduli na Karatu ambapo mgogoro upo mpaka sasa #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-Nimestaafu siasa ina maana sina Chama lakini haimaanishi sina nchi, nitabaki kuwa mtetezi wa wanyonge #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr. WILBROD SLAA-Nimeombwa kugombea Urais karibu vyama vitano nimekataa kwa kuwa siamini wala sitaki kuyumbishwa #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
DR.WILBROD SLAA-Najua hela za ROSTAM AZIZ ndio zinasaidia mambo ya uchaguzi, pesa zinagawanya kila kona ya nchi #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Hakuna kipindi nimepata vitisho kama hiki, hata kipindi cha kutaja List of shame haikuwa hivi #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr WILBROD SLAA- ‘Kama kuna Maaskofu mmehongwa nchi hii ni bora mkaenda mbele za Mungu kutubu na kuomba msamaha #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-Narudia tena siendi wala sitakwenda chama kingine chochote nitakuwa Mtanzania wa kawaida kama wengine #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr WILBROAD SLAA-Namtaka LOWASSA leo atoke hadharani atuambie Richmond ni ya Nani? na huyo mkubwa ni nani? si kazi rahisi #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr WILBROD SLAA-‘Nataka ripoti ya Richmond iwekwe hadharani ili wale wanaopiga propaganda waadhirike ili watu wawaelewe #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr WILBROAD SLAA-Sina sababu ya kurudisha kadi, ni sawa na kadi ya ndoa,ni mali yangu, ni kumbukumbu katika maisha yangu #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr. WILBROD SLAA-Sina ugomvi na MBOWE ni vyema nikasema, hata nyumba ninayoishi alinisaidia, itakuaje niwe na chuki naye #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-CCM wanilitaka niachie jimbo la Karatu mwaka 2000, nikawaambia sharti saini 3, ya Rais, yangu na ya YESU #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
DR WILBROD SLAA- Nilimshukuru Mungu kutokwenda CCM kwa sababu ningefukuzwa ndani ya miezi mitatu kwa kuwa nisingekubali #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
DR WILBROD SLAA-Simpigii kampeni mtu yoyote lakini nimefanya utafiti kuona Taifa litapata hasara gani akichaguliwa LOWASSA#MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr WILBROD SLAA-Niliambiwa nina dk5 za kuishi, piga magoti muombe Mungu wako akusaidie baada ya kutaja ufisadi wao #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje? #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr.WILBROD SLAA-‘Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje? #MillardAyoUpdates
— millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
Dr. WILBROD SLAA-‘Silaha huziweki zote mezani, nimewaomba wahusika wajitokeze, wakifanya hivyo nitarudi tena kuzungumza #MillardAyoUpdates — millard ayo (@millardayo) September 1, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikiaza siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos