Washiriki wa Kili Music Awards wametangazwa March 25 2014 ambapo ndani ya washiriki hao kuna watatu nyimbo zao zimefutwa na BASATA sababu ya kukosa maadili ya kitanzania ukiwemo wimbo wa ‘nimevurugwa’ wa Snura.
Snura ameongea na millardayo.com na AyoTV na kuelezea hisia zake baada ya kusikia hiyo taarifa akianza kwa kusema >>> ‘Sio nimevurugwa peke yake hadi ‘majanga’ nao haukuingia’
‘Labda niuzungumzie wimbo wa Nimevurugwa kama ambavyo wamesema hauna maadili, kitu kimoja ambacho watu wanatakiwa kukifahamu si kwamba wimbo hauna maadili hata kidogo, wimbo wa Nimevurugwa ni wimbo mkubwa kwanza unaofundisha na ndani yake nimeimba mambo yanayoihusu jamii’
‘Nadhani waliousikia wameelewa ule wimbo nimeimba nini ila video niliyofanya labda kutokana na mimi kukata viuno sana kwa hiyo video ndiyo maana wamesema haina maadili na ndiyo maana video ikafungiwa lakini uamuzi huu usiwe kwa audio, kwenye tuzo kuna category nyingi sana na ndiyo maana kuna category ya wimbo bora na video bora’
‘Inawezekana wimbo ukawa mzuri ukapata tuzo na inawezekana video ikawa sio nzuri ikakosa tuzo lakini kwenye wimbo wa ‘nimevurugwa’ ilikua inastahili wimbo kama wimbo uingie ila video iachwe kwa sababu haina maadili’
‘Nimekua na kijiswali kinachonitatiza kichwani mwangu inawezekana haya mambo sijayaelewa vizuri labda nimeingia kwenye category ya msanii bora chipukizi wa mwaka 2013 ni kipi ambacho nilikifanya kizuri kilichopelekea mimi kuingia hapo?’ – Snura
‘Nauliza hivyo kwa sababu sikuingia kwenye utumbuizaji bora wala hakuna nyimbo yangu yoyote iliyoingia kuwania tuzo si majanga wala nimevurugwa, sasa hapo kidogo pananitatiza sijui ubora wangu umetokea wapi hadi kuingizwa kwenye chipukizi?’