Club ya Hertha Berlin ya nchini Ujerumani imemsimamisha mshambuliaji wake wa kimataifa wa Ivory Coast Solomon Kalou baada ya kuonekana kwa video ikimuonesha akipuuza agizo la socila distance na kuamua kuwapa mikono wachezaji wenzake na trainer wake.
Kalou katika video hiyo aliyokuwa ana stream LIVE kupitia facebook account yake imesambaa na inawezekana ikaiweka matatizoni zaidi Ligi Kuu ya Ujerumani ambao imepangwa kurejea May 15 baada ya kusimamishwa toka March 8 sababu ya janga la corona.
Hata hivyo Chancellor wa Ujerumani Angela Markel amepanga kutangaza njia mbadala itakayoiwezesha Bundesliga kurejea pasipo kuleta madhara au kuongeza idadi ya maabukizi ya virusi vya corona, uamuzi huo utatangazwa May 6 2020.
AUDIO: UJERUMANI MKIKUTWA ZAIDI YA WAWILI NA HAMUISHI NYUMBA MOJA, FAINI TSH LAKI 7