Mwigizaji Steve Nyerere aamua kumuomba radhi mwimbaji Ommy Dimpoz baada ya kusema kuwa hatoimba tena kutokana na hali yake kutokua nzuri kipindi alichofanyiwa operesheni ya koo nchini Afrika Kusini.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Steve Nyerere ameomba radhi na kufafanua baadhi ya maneno yake aliyoyasema na hii ni kutokana kuwa na maneno mengi yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya watu kufanya kauli yake kama kichekesho.
“Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru M/Mungu, lakini pili nichukue fursa hii kumuomba radhi ndugu yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake. Na zaidi niwaombe radhi Watanzania wote na wapenzi wa sanaa.
Binadam unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea nami nakiri kukosea kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz”
“Lakini ifahamike kwamba kauli ile haikuwa kwamba namtakia mabaya Dimpoz HAPANA, ila kwa tulivyokuwa tunapata taarifa kwakweli zilikuwa zinatukatisha tamaa.
Mengi yanaongelewa lakini mfahamu kwamba sikuwa na nia mbaya au nilikuwa na ugomvi na ndugu yangu huyu bali kama binadam hutokea kuteleza kwenye kuzungumza hivyo nawaomba suala hili lisichukuliwe kwa nia mbaya HAPANA”
“Lakini tufahamu kwamba M/Mungu hufanya miujiza yake kutokana na sababu fulani, hivyo miujiza ya kumuinua ndugu yetu na kurudi kwenye kazi zake imetokana na imani aliyokuwa nayo Dimpoz kwa Muumba wake”
“Najua mie niliteleza kusema kwamba Dimpoz hatoimba tena lakini sikuwa na nia hiyo, kwamba natamani Dimpoz asiimbe tena HAPANA. Hivyo pamoja na vichekesho mbalimbali vinavyotolewa juu yangu mie nafurahi sana kwani vinazidi kuupaisha wimbo mpya (NI WEWE) wa ndugu yangu na napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania na wapenzi wa mziki kumsupport ndugu yetu na kuzidi kumuombea dua kwa M/Mungu azidi kuimarika kiafya. AMIN🙏”
MWANZO MWISHO: ALIETENGENEZA ‘NI WEWE’ YA OMMY DIMPOZ KAFUNGUKA YALIYOTOKEA STUDIO