Leo February 26, 2019 Staa wa R&b R Kelly ameachiwa kutoka gerezani kwa Chicago Marekani baada ya kulipa dhamana ya zaidi ya Milioni 200 za Kitanzania, msemaji wa idara ya polisi ameeleza.
Mapema Jumatatu alikana mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wanne, watatu kati yao walikuwa ni watoto wakati wa uhalifu huo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 52 alionekana akiwa amevaa koti la samawati, hakuzungumza na waandishi habari aliposindikizwa kutoka gerezani na Wakili wake. Alijisalimisha kwa polisi Ijumaa na alisalia gerezani wikendi nzima.
Muimbaji huyo amekabiliwa na tuhuma za unyanysaji kwa miaka kadhaa bila kushtakiwa , na amekana tuhuma zote za awali.
Mama wa Kijana alietengeneza Pikipiki azungumza ’’Hatuna uwezo wa kumsomesha”