Nimekutana na hii mtu wangu list ya wachezaji soka ambao majina yao yana maana tofauti na yanachekesha sana ukiyasoma. Wakati mwingine kama unaweza kumuita mchezaji mbele za watu wasio mfahamu wanaweza kujua una maana tofauti, mfano kuna mchezaji anaitwa Drinkwater kwa kiswahili ni kunywa maji. Hii nimeikuta sokkaa.com.
4- Argelico Fucks huyu ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil ambaye amewahi kuitumikia klabu ya FC Porto na sasa ni kocha wa Sporting Lisbon. Jina lake la pili huwa halitafsiriwi kwa maana nzuri, sijui kama unamuita hadharani kwa watu wasiojua kuwa ni jina lake watashangaa.
3- Danny Drinkwater anakipiga katika klabu ya Leicester City ya Uingereza, jina la pili lina maana ya kunywa maji, hivyo ukichanganya jina lake la kwanza la pili halafu ukitafsiri utapata maana ya “Danny kunywa maji”
2- Johnny Moustache huyu ni mchezaji soka kutoka visiwa vya Seychelles jina lake la pili lina maana ya ndevu za juu ya mdomo hivyo kama utamuita jina lake hilo watu huenda wakafikiria ni jina la utani.
1- Danger Fourpence kama utakuwa unasikiliza mpira katika radio halafu ukasikia mtangazaji wa radio ya kiingereza ana tamka jina lake la mwanzo huenda ukafikiri sio jina lake ila anaeleza kuwa ni hatari uwanjani. Licha ya kuwa na jina hilo Danger Fourpence ambaye anatokea Zimbabwe anatajwa kutokuwa hatari sana uwanjani tofauti na jina lake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.