Kundi kubwa la watalii wapatao 17 kutoka nchini ufaransa wametembelea mgodi wa kuzalisha madini aina ya Tanzanite katika mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na kampuni ya franone Maining ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
Kundi hilo ambalo ndani yake wapo wataalamu wa kukata na kuongeza thamani ya madini pamoja na wanafunzi wa kuongeza thamani ya madini wamesema wamefurahia kuona sehemu pekee inayo chimbwa madini ya Tanzanite ambapo ni Mkoa wa manyara wilayani Simanjiro mkoani Manyara .
Akiongea mara baada ya kupokea kundi ilo meneja mkuu wa kampuni ya Franone Mining Vitus Ndakize amesema wamejisikia faraja kubwa sana kwa wageni hao kufika katika mgodi pekee mkubwa yanapo patikana madini aina ya Tanzanite .
Serikali ilitangaza tenda mwaka 2022 mwezi wa wa nne ambapo kampuni ya franone Mining ilishinda tenda hiyo mwezi wa sita na kupewa leseni ya uchimbaji mwezi wa saba mwishoni huku serikali ikiwa na ubia asilimia 16 na mpaka sasa umeanza kazi za uchimbaji ikitegemea kuanza uzalishaji wa madini ya Tanzanite wakati wowote.