Michezo

Stand United wako vizuri, wamemvuta Kocha wa Simba? Usipitwe na hii…

on

Hii itakuwa mara ya pili kwa Kocha Patrick Liewig kupata dili la kufundisha Klabu ya soka Bongo, aliwahi kuifundisha Simba Sports Club mwaka 2013 na baadae akatimua, karudi tena Bongo?

SONY DSC

Patrick Liewig enzi hizo akiwa kwenye uzi wa Simba.

Klabu ya Stand United ya Shinyanga imemleta kocha kutoka Ufaransa Patrick Liewig kuwa Kocha wa kikosi hicho.. Liewig ametangazwa leo kuwa mwalimu wa kikosi hicho na atasaini mkataba wa miaka miwili na kuungana na kocha Martin Lule.

Liewig anaangaliwa kwa jicho la tatu kwamba atasaidia kuinua kiwango cha timu hiyo ambayo katika Ligi Kuu msimu uliopita ilimaliza ikiwa nafasi ya 10 na iliambulia point 31 baada ya kucheza mechi 26…. Stand United ambayo imedhamiria kuleta ushindani msimu ujao itashiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania bara kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kupanda daraja.

Stand United imeimarika kiuchumi baada ya kuingia mkataba wa udhamini wenye thamani ya bilioni 2.4 kwa kipindi cha miaka miwili na kampuni ya uchimbaji madini… Hata hivyo Patrick Liewig anarudi tena TZ kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza aliwahi kuwa kocha wa Simba kuanzia January 6 2013 hadi Desemba 31 2013.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments