Stan Bakora kwa sasa yuko kwenye headlines za wachekeshaji ambao wanapendwa kulingana na vichekesho vyao Tanzania,yeye vichekesho vyake anafanya na Rafiki yake Kitale ‘Mkude Simba‘
Style anayotumia Stan Bakora kuchekesha ni ile ambayo anaonekana anajibishana na Kitale lakini kwa lafudhi ambayo kama ukimsikia vibaya unaweza kuhisi ni Rappa Ney wa Mitego.
Ney wa Mitego na Stan Bakora kumbe wanafahamiana siku nyingi leo Stan anatupa stori kuwa kuna siku ambayo Ney wa Mitego alichelewa kwenda kwenye show akawa amewatanguliza Stan Bakora na wenzake ili wahusika waamini kuwa atafika.
Walipofika mkoa ambao Ney alikua anafanya show wakati wanatoka hotelin wakati anaongea wakamuuliza ‘Wewe ndio Ney?’ anasema aliogopa kujibu ndiyo yeye kwa sababu alikua na hofu ya kupigwa akawajibu ‘Ney mwenyewe anakuja‘.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.