Soka ni mchezo unaopendwa duniani kote na imezoeleka kwamba ni mchezo ambao mara nyingi hufuatiliwa na watu daraja la kati na daraja la chini huku watu wa daraja la juu ambao wengi ni matajiri na watu maarufu wakiwa hawana muda wa kufuatilia mchezo huu.
Hata hivyo ukubwa wa soka unaweza kuwa umetazamwa kwa jicho la kawaida kwa uhalisia ni kwamba nguvu ya mchezo huu ni kubwa kiasi kwamba hata watu maarufu wameshindwa kuepuka wingu la ushabiki wake.
Katika hali ya kawaida ligi ya England ndio ligi inayopendwa na kufuatiliwa na idadi kubwa ya watu duniani na timu zake kubwa kama Manchester United, Arsenal, Liverpool na Chelsea zikiwa na idadi kubwa ya mashabiki nje ya England kuliko hata klabu za Barcelona na Real Madrid.
Labda utashangazwa kwamba kuna idadi kubwa ya mastaa DUNIANI ambao wanaufuatilia mchezo wa soka kuliko ambavyo watu wengi wanatarajia.

Waziri mkuu wa England, David Cameron pamoja na kutingwa na shughuli za siasa ni shabiki wa kutupwa Aston Villa.
Cameron anaungwa mkono katika ushabiki wake wa klabu hii na mjukuu wa Malkia Elizabeth, Prince Harry ambaye ni shabiki wa Aston Villa pia .
Baba yake Prince Harry ambaye ni Prince Charles yeye ni shabiki wa Burnley F.C klabu ambayo rangi za jezi yake inafanana na rangi za jezi ya Aston Villa.

Nyota wa muziki wa Pop, Justin Bieber yeye amethibitisha kuwa shabiki wa klabu ya Everton na amepigwa picha akiwa na jezi za klabu hiyo huku akicheza mpira na wenzie.

Staa wa Hip Hop ambaye ana urafiki na Rais Obama pia, Jay Z hayuko nyuma kwenye masuala ya soka na amekiri kuwa shabiki mkubwa wa klabu ya jijini London ya Arsenal.






Kaa karibu na millardayo.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia hii itakufikia >twitter Insta Facebook