Ahadi nyingi zilitolewa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani ambapo sio tu kutoka kwa Wagombea bali hata mastaa wakubwa waliokuwa upande Hillary Clinton, wengi waliahidi kuondoka Marekani na kuhamia mataifa mengine iwapo Donald Trump atashinda.
Tayari matokeo yametangazwa jana November 9, 2016 na kuonyesha kuwa Donald Trump ndiye mshindi na Rais mteule wa Marekani ambaye ataapishwa kuwa Rais kamili wa taifa hilo January 20, 2017.
Mastaa watano walioandika watahama nchi ni hawa hapa kwenye hii orodha akiwemo mwimbaji Miley Cyrus yeye alisema “I am moving if he is president. I don’t say things I don’t mean!” ‘Nitaondoka kama Trump atakuwa Rais, huwa siongei vitu ambavyo simaanishi.’
Baada ya mastaa hao kuyaongea hayo, raia wa Marekani wanasubiri kuwaona watafanya kweli baada ya Trump kuchaguliwa kuwa raisi wa 45 wa Marekani.
VIDEO: Uliikosa hii? Pesa aliyolipwa Diamond Platnumz baada ya video yake kuchezwa kwenye TV Marekani? bonyeza play hapa chini
VIDEO: Uliikosa hii? Tazama Mtanzania Mayunga alipofika nyumbani kwa Akon Marekani, bonyeza play hapa chini