Michuano ya Euro 2016 bado inaendelea lakini kubwa ambalo limeingia kwenye headlines leo June 20 2016 ni kuhusiana na ubora wa jezi walizotumia timu ya taifa ya Uswiss katika mchezo dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Ufaransa.
Uswiss walivaa jezi ambazo zilikuwa zinachanika wakati wa mchezo, endapo tu mchezaji wa Uswiss atavutwa jezi na mchezaji wa Ufaransa, kiasi ambacho kilipelekea winga wa Stoke City ya England anaichezea timu ya taifa ya Uswiss kutoa kauli ya kejeli kuwa “hafikiri kuwa Puma wanatengeneza Condom”
Leo June 20 kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma ambao ndio watengenezaji wa jezi hizo, wametoa kauli ya wameanza kufanya uchunguzi, kutokana na ubora jezi hizo kuwa dhaifu, Uswiss ilifanikiwa kufuzu hatua ya mtoa baada ya kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A kwa kutoka sare ya 0-0 na Ufaransa.
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUB