August 10 2016 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani (Ubungo terminal) na kubaini mapungufu kadhaa ikiwemo ubadhirifu wa tiketi pia amesema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho wa kuihamishia stendi hiyo kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.
‘Shahuku yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo‘ –Paul Makonda
‘Nataka kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli yanabeba ngano na makontena‘ –Paul Makonda
‘Lakini kabla ya wiki hii haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka, sitaki kuviona vifusi katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20 nitarejea kujionea utekelezaji wake kama umekamilika‘ –Paul Makonda
‘Kuanzia leo ni marufuku mtu kupiga faini katika parking ya ubungo, lazima tuweke alama za eneo gani la kupaki na wapi sio eneo la kupaki na hili itaanza baada ya kukamilika kwa ugawaji wa maeneo hayo‘- Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA MATATU YA MAKONDA KUHUSU DAR ES SALAAM