Haya mtu wangu wa nguvu wakati tunaendelea kusherehekea sikuku ya mwaka mpya 2016, ninayo list ya style 9 za nywele zilizotamba kwa mastaa wa soka wa Ulaya kwa mwaka 2015. Stori kutoka 101greatgoals.com inawataja mastaa hawa ndio waliokuwa na style za nywele zilizotamba. Miongoni mwa mastaa waliotajwa ni Iniesta, Raheem Sterling na Paul Pogba.
1- Raheem Sterling aliwashangaza wengi baada ya kuingia uwanjani kupasha misuli moto katika mchezo kati ya Man City dhidi ya Leicester City akiwa na style ya nywele ya tofauti na watu walivyomzoea. Sterling aliweka dred fupi na kuwa katika muonekano kama wa shujaa wake Whoopi Goldberg.
2- Andres Iniesta wa FC Barcelona huyu alishangaza wengi baada ya kuingia uwanjani akiwa na muonekano tofauti wa nywele kichwani katika michezo ya fainali ya klabu Bingwa Dunia iliyofanyika December Japan.
3- Paul Pogba wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa aliingia kwenye headlines baada ya kuweka au kunyoa kiduku lakini pembeni ya kichwa chake kukiwa na michoro ya muziki, hii ilikuwa mwezi November na ilitajwa kama moja kati ya style za nywele za kibunifu kuwahi kutokea.
4- Kiungo wa Man City Samir Nasri yeye alibadili muonekano wake wa nywele mwezi October baada ya kubadili rangi ya nywele zake kutoka nyeusi na kuziweka katika muonekano wa rangi ya kijivu.
5- Beki wa klabu ya FC Barcelona Dani Alves yeye anatajwa kupewa tuzo ya kunyoa style mbaya kuliko wote kwa mwaka 2015. Hii ilikuwa mwezi May lakini watu wakaanza kutafuta ni style ipi mbaya kuwahi kunyolewa zaidi ya hiyo.
6- Kwa sababu Andy Carroll anatajwa kuwa style hii ya nywele haikumpendeza, baada ya watu kadhaa wa soka kuiponda na yeye pia alijutia kufanya maamuzi hayo.
7- Kwa mwaka 2015 ile style ya unyoaji ya Ronaldo de Lima alionyoa katika fainali za Kombe la Dunia 2002 ilichukua nafasi baada ya Fernando kunyoa akiwa anakipiga katika Ligi Kuu Uturuki.
8- Kiungo wa Rome mwenye umri wa miaka 35 Ratinho aliingia kwenye headlines mwezi April baada ya style yake ya nywele kichwani kuwa ngeni machoni mwa watu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.