Naibu wa kwanza wa Rais nchini Sudan Kusini Rieck Machar amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona, taarifa kutoka Ofisi ya Machar iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuthibitishwa na Msemaji wake James Gatdek Dak, mke wa Machar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi Angelina Teny pamoja na watumishi kadhaa wa ofisi yake na walinzi pia wamekutwa na maambukizi.
Machar mwenyewe ametoa taarifa kwa umma kwamba ameambukizwa virusi vya corona na kuanzia leo atajiweka karantini kwenye makazi yake kwa siku 14 zijazo.
Kulingana na takwimu za wizara ya afya ya Sudan Kusini zilizotolewa hapo jana, hadi sasa kumerekodiwa visa 339 vya COVID-19 na vifo sita.
Ingawa idadi hiyo ni ya chini lakini ni watu 3,908 tu ndio waliopimwa. Mashirika ya misaada yamekuwa yakielezea wasiwasi kuhusiana na kuongezeka kwa haraka kwa visa hivyo katika siku za karibuni nchini humo.
Via DW.
SPIKA AMVAA TENA KAFICHUA MAZITO “WANATEKA WABUNGE WAO, ANAWAFANYA ANAVYOTAKA”