Mh. Frederick Sumaye akihojiwa na Maestro wa Sports Extra ya Clouds FM picha ikiwa imepigwa na http://michuzijr.blogspot.com ambapo kwenye Exclusive interview na millardayo.com Frederick Sumaye ndio ameyatoa yake ya moyoni hapa chini.
1. ‘Tatizo langu la kwanza ni kwamba tumewafikisha Watanzania mahali ambapo tunafikiri wakipata katiba mpya ndio jawabu la matatizo yao, ukiangalia sana watu waliokua wakitoa maoni hatukuwapa elimu ya kutosha juu ya katiba kwa hiyo walikua wanaeleza machungu wanayoyapata kwenye maisha wakifikiri yanasababishwa na katiba hivyo ikipatikana mpya haya yatatoweka kitu ambacho sio kweli’
2.’Katiba mpya haitatatua matatizo yao kama wanavyofikiria, kitakachotatua matatizo yao ni usimamizi mzuri wa sera na sheria zetu, kama tutasimamia vizuri hayo hata kama katiba ingekua ya karatasi moja nchi bado itakwenda mbele’
3. ‘Katiba hata ungeitengeneza leo……. baada ya miaka mitano, miwili au mitatu itaanza kuwa na marekebisho kwa sababu jamii haijaganda.. katiba zile ambazo hazibadiliki sana duniani kama ukizichunguza ni zile ambazo haziweki kila kitu kwenye katiba yani kama kuna mabadiliko kwenye jamii ni sheria tu zinabadilika ila katiba inabaki palepale’
4. ‘Na neno viraka sio sahihi, hili ni neno tu ambalo linatumika na wale ambao hawaitaki katiba hii kwa sababu yeyote’
5. ‘Katika mfumo wa serikali hizi mbili tuna matatizo mawili… la kwanza, unaona kabisa kuna hali fulani ya misuguano ya kimadaraka na ndio inajenga kitu kama chuki au kutoridhika dhidi ya upande mwingine, ukienda kwa upande wa Znz wanayo mambo mengi dhidi ya upande wa bara na ukienda kwa Wabara nao wana mambo mengi wanayolalamikIa dhidi ya Wazanzibari, kama hatujatatua hayo katika serikali mbili, serikali ya tatu haiwezi kutatua, ndio itayazidisha’
6. ‘Nikupe mfano hai, Zanzibar wana wimbo wa taifa, Rais wao, bunge lao wana serikali yao na Rais wao anapigiwa mizinga 21 kama Rais wa Jamuhuri ya muungano, zamani hayo hayakuepo yamekuja taratibu tu ndio maana nasema kama kuna mvutano flani hivi’
7. ‘Hayo katika mfumo huu wa serikali mbili ungeweza kusema hayapendezi sana….. sasa utakapoweka serikali ya tatu ya Tanganyika, inamaanisha Tanganyika itakua na wimbo wake wa taifa, serikali yake, bunge lake, wimbo wake wa taifa, Rais wake pia atapigiwa mizinga 21…… yani kule Zanzibar Rais wake anapigiwa mizinga 21, huku anapigiwa mizinga 21, na huyu unaemuita bwana mkubwa anapigiwa mizinga 21′
Hayo ndio maoni ya Frederick Sumaye aliekua waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwenye awamu ya tatu iliyoongozwa na Benjamin Mkapa.
Baada ya kumsoma, maoni yako ni yapi kuhusu katiba na alichosema? share na mimi hapa chini kwenye comment mtu wangu pia ungana na mimi facebook, twitter na instagram kwa jina la Millard Ayo ili kuwa mwanafamilia wa millardayo.com na kupata matukio yote kwa haraka zaidi.