Wacheza soka wengi huwa wanaishia kufanya biashara au kuwa Makocha baada ya kustaafu kucheza soka ila hawa ni miongoni mwa wachache walioamua kuingia kwenye dini na kuwa Wahubiri.
1. Taribo West
Mchezaji matata wa Super Eagles alihadithia alivyojihusisha na mambo ya kishetani alipokuwa Mchezaji, alikutana baadae na Mchungaji wa kike, Patience Ikemefuna aliemwambia neno la Mungu na akambadilisha, mpaka sasa ni Mchungaji na mwanzilishi wa Kanisa la Shelter in The Storm Miracle Ministries of All Nations.
2. Peter Knowles
Mchezaji wa Wolverhampton Wanderers, alijiunga na kanisa la Jehovah’s Witness mwaka wa 1969.
3. Phil Mulryne
Nyota wa Manchester United ambaye alitawazwa kuwa padre wa Katoliki Jumamosi Julai 8, 2017, alikuwa mmoja wa Wachezaji wa mwanzo wa Sir Alex Ferguson mwaka 1997.
4. Gavin Peacock
Gavin aliichezea New Castle na alikuwa kapteni Chelsea kuanzia mwaka 1984 hadi 2002 ambapo baada ya kusomea theolojia sasa ni Mzee na Mchungaji wa Kanisa la Calvary Grace Church, Calgary.
5. Chase Hilgenbrinck
Huyu ni raia wa Marekani alicheza kama ‘defender’ katika klabu ya Ñublense na New England Revolution kabla ya kustaafu mwaka 2008 akiwa na miaka 24 ili awe Padri
6 Alan Comfort
Alijiunga na Wakristo akiwa na miaka 20 akiwa Chuo Kikuu cha Cambridge ambapo alisomea Upadri katika Kanisa la Anglikana, huyu aliwahi kuzichezea Middlesbrough na QPR.
HD VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOTANGAZA KUWASAMEHE BABU SEYA NA PAPI KOCHA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA