Michezo

Mwinyi Zahera hajafurahishwa na uamuzi wa game yao kuchezwa saa 8 mchana

on

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera muda mchache kabla ya kuanza kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri Morogoro, amelalamikia uamuzi wa kupanga mechi hiyo ichezwe saa nane mchana wakati jana hakukuwa na michezo ya AFCON, Mwinyi Zahera kayaongea hayoa akihojiwa na Azam TV kabla ya game kuanza.

“wachezaji wanachoka sio gari, Kwa sababu gani tunacheza saa nane kwa nini tusingecheza jana hakukuwa na AFCON, wakati tumecheza mechi muda kwa nini tusicheze jana, AFCON ratiba imepangwa miezi saba iliyopita lakini kwa nini tucheze leo saa nane”>>>Mwinyi Zahera

Yanga na Simba SC zote zinaingia uwanjani kucheza saa nane mchana katika viwanja viwili tofauti, wakati Yanga wapo katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Simba SC wapo ugenini Tanga kucheza dhidi ya Costal Union.

Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?

Soma na hizi

Tupia Comments