Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mtanzania Askwari Hilonga ambaye ni Mhadhiri wa Chuo cha Nelson Mandela, Arusha ambaye ameshinda tuzo tano kwa kutengeneza mtambo wa kuchuja maji kuondoa vijidudu bila kutumia kemikali.
Hilonga amedai kuwa kutokana na ugunduzi huo ametoa ajira kwa vijana kadhaa huku lengo lake likiwa ni kuajiri vijana Mia Moja ambapo ana uwezo wa kuingiza kipato cha Tsh. Milioni Tano kila mwezi.
>>>”Huu mtambo umenipatia umaarufu sana. Nimeshinda Tuzo Tano duniani mojawapo ni Tuzo ya Africa Price for Engineering Innovation. Nilikuwa mshindi na nikazawadiwa Milioni 80 ikanisaidia kuanzisha Kampuni yangu.” – Askwari Hilonga.
ULIKOSA? Tumbo limetobolewa lakini anatembea!!!
Teknolojia ya Panya kutoka Tanzania ambayo inashinda za wazungu