Bondia Floyd Mayweather amemchana Rapa T.I na kusema hana mpango wa kumchukua mke wake na kwamba anashangazwa na jinsi Rapa huyo alivyoanzisha ugomvi nae kwasababu alidhani wote ni marafiki tu.
Story ni kwamba Floyd anasema kuwa hajawahi kufikiria kuwa kulikuwa na “beef” kati yake na T.I na pia hataki hata kujiingiza katika mahusiano yoyote ya kimapenzi na mke wa T.I, bibie Tameka.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Mayweather amekasirishwa sana na kitendo cha kusingiziwa kuiba mke wa mtu na kusema ni ujinga kwa T.I kumchukia bila sababu ya msingi kwakuwa ni Tameka mwenyewe aliyetaka kula bata na Mayweather huko Vegas.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.