Bondia Hassan Mwakinyo kwa mujibu wa video inayosambaa mtandaoni, amemuonesha uwezo wake tena kijana anayejulikana kwa jina la Mpemba ambaye alimfuata usiku wa April 14 2019 kumuomba wapimane ubavu akiamini kuwa yuko vizuri kupambana na Hassan Mwakinyo kwa wakati huo.
Mwakinyo akiwa kwao alimuona kijana huyo na kusisitizia kuwa lile ombi lake alilokuwa kaongea nae mapema, ndio amekuja kulitekeleza la kupamba na Mwakinyo “Ilikuwa mida kama ya saa tatu usiku nilienda sokoni kununua maziwa na mshikaji wangu nikakutana nae akaniambia bwana mimi nataka kuja kujipima na wewe siku moja nikamuuliza lini umepanga akaniambia siku yoyote tu”
Kutokea Algeria, Morocco na Hispania Ulimwengu, Msuva na Chilunda kuhusu Kundi C AFCON 2019