Usiku wa UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 umeendelea kuwa ni usiku wa maajabu kutokana na kila mchezo kuleta matokeo ya kushangaza na yasio tarajiwa na wengi, baada ya club ya Liverpool ya England kufuzu kucheza fainali kwa kupindua matokeo dhidi ya FC Barcelona, May 9 ilikuwa ni zamu ya kuishuhudia nusu fainali ya pili ya marudiano.
Tottenham Hotspurs baada ya kupoteza kwa goli 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Ajax waliowashangaza wengi msimu huu wakiwa wanaaminika kama under dog, leo wamekutana na matokeo ya kushangaza dhidi yao wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, Ajax aliingia katika mchezo wa marudiano akiwa tayari na faida ya goli moja alilolipata katika mchezo wa kwanza ugenini.
Ajax mapema kabisa kipindi cha kwanza wakaanza kwa kuikatisha tamaa Tottenham kufuatia kuifunga magoli mawili ya utangulizi kupitia kwa De Ligts dakika ya 5 na Zerich dakika ya 36, hivyo mchezo ukaendelea kuwa mgumu zaidi kwa Tottenham, hali ya upepo ilibadilika kuanzia dakika ya 55 kipindi cha pili Lucas Moura alipofunga goli la kwanza la Tottenham kabla ya dakika 3 baadae kufunga la pili.
Magoli mawili ya mapema yalirudisha morali kwa Tottenham na kujikuta kuongoza juhudu, kwani walikuwa wanahitaji goli moja tu kufuzu huku wenzao Ajax wakionesha kuanza kucheza mchezo wa kupoteza muda kitu ambacho kilikaribia kufanikiwa, ukiwa mchezo unaelekea kumalizika dakika ya 5 ya nyongeza inamalizika Dele Ali akatoa pasi nzuri kwa Lucas Moura na kufunga hat-trick iliyoipeleka Tottenham fainali.
Dakika 90 zikamalizika kwa Spurs kupata ushindi wa 3-2 ila Spurs pamoja na kuwa aggregate sawa ya magoli 3-3 dhidi ya Ajax, Spurs wanafuzu kutokana na Ajax kuruhusu magoli mengi nyumbani, game ya fainali itakuwa inazikutanisha timu zote za England June 1 2019 katika jiji la Madrid Hispania uwanja wa Metropolitano, ila ushindi huo wa Spurs unazifanya club za England zilizowahi kufika fainali ya UEFA Champions League kuwa nane hakuna taifa lolote lililowahi kufikia rekodi hiyo.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania