March 8, 2017 ni siku ya wanawake duniani ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameyaandika haya.
‘Asilimia kubwa ya Wanawake ni aina ya watu waliokuza watoto wao katika mazingira magumu, mateso, machungu na kunyanyasika kwa hali ya juu mara nyingine, na walikubali kupitia hayo ili tu mtoto asimame na kuwa mtu atakaejitegemea na kutegemewa siku moja’- Paul Makonda
‘lakini kuna kundi kubwa lililodhamiria kwa makusudi kabisa kuwarudisha nyuma kwenye mategemeo yao hayo, kundi lililopanga kwa makusudi kabisa kuangamiza vijana wao kwa ajili ya maslahi yao binafsi’-Paul Makonda
‘Kundi lisilojali kwa namna yoyote struggle za kina mama hawa katika kuwakuza watoto wao, kundi linalowaharibu huku wakiwa wanajua kabisa athari kwa tamaa tu ya mali za haraka. Kundi la wauzaji wa dawa za kulevya’
‘Siku ya leo tunapoadhimisha siku ya Wanawake duniani napenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia kina mama wote na wananchi wa mkoa wangu wa Dar es Salaam kuwa sitakubali watoto mliowabeba matumboni mwenu miezi tisa na kuwalea kwa tabu wafe kwa matumizi ya madawa ya kulevya’. Paul Makonda
‘Naomba tuungane na Mheshimiwa Rais wetu Magufuli kuhakikisha tunashinda dhidi ya wauaji na wanyonyaji wanaofanya biashara haramu ya dawa za kulevya. Kama uliweza kumtunza tumboni miezi tisa basi usikubali mtoto wa mwingine akakatisha matumaini yako, mlinde mwanao ili ule matunda ya uzao wako’- Paul Makonda
ULIIKOSA HII YA MKUU WA MKOA WA DSM PAUL MAKONDA ALIVYOKWENDA KWENYE KANISA LA KKKT BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA