Simba SC imeomba kibali kwa jeshi la polisi kufanya maandamano siku ya Jumanne ya April 25 2017 kutoka Makao makuu ya Club hiyo Msimbazi hadi wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo kukutana na waziri Mwakyembe, leo viongozi wao wamekutana na waziri Mwakyembe.
Jumanne ya tarehe 25 2017 itakuwa ni siku ya wanachama na mashabiki wa Simba wakati leo ilikuwa ni zamu ya viongozi wao ambapo walikutana na waziri, naibu waziri na katibu mkuu wa wizara hiyo, viongozi wa Simba waliyokwenda wizarani leo ni Rais wa Simba Evans Aveva, makamu wa Rais Geofrey Kaburu.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe na Said Tuli ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, bado Simba hawajasema zaidi walichozungumza na waziri lakini taarifa zinaeleza kuwa ni juu ya uendeshwaji wa soka na TFF ambapo kwa upande wao wameona hawafanyiwi haki.
VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar