Asubuhi ya August 4 2016 taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Rais wa Simba Evans Aveva kutiwa mikononi mwa Polisi kutokana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuagizwa kukamatwa kwa kiongozi huyo.
millardayo.com ilifuatilia kwa kina kuhusiana na taarifa hizo na kufanikiwa kumpata kaimu afisa msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli na kuweka wazi kuwa kilichomfanya Rais wa Simba kukamatwa ni tuhuma za uchepushwaji wa pesa za usajili za mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Emmanuel Anord Okwi kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia.
“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya TAKUKURU kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, tuhuma zinazomkabili ni uchepushwaji wa fedha kutoka account ya Simba kwenda katika account yake na baadae kuanza kufanyiwa mgawanyo katika account nyingine, ni fedha za usajili wa Okwi kutoka Etoile du Sahel”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba mwaka 2013 na kujiunga na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho wa zaidi ya Tsh milioni 450, malipo yalicheleweshwa kulipwa hadi FIFA walipoingilia kati na mwaka huu malipo ndipo yalikamilika.
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2