Michezo

Hii ndio rekodi nyingine aliyoiweka Amissi Tambwe wa Simba

on

IMG_6391MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Burundi, Amissi Tambwe ameweka rekodi ya pekee ya kwanza baada ya kufunga mabao 17 sawa na namba ya jezi anayoitumia tangu atue kuichezea timu hiyo.

Tambwe ndiye anayeongoza kwenye orodha ya ufungaji katika msimu huu baada ya kufikisha idadi hiyo ya mabao akifuatiwa na kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche mwenye mabao 11 na mshambuliaji wa Ruvu Shooting, Elius Maguri amefunga mabao tisa.

Idadi hiyo ya mabao iliwahi kufikiwa na Tchetche msimu uliopita na kuwa mfungaji bora, mbali na hilo pia mshambuliaji huyo ndiye pekee aliyeweka rekodi ya kupiga hat-trick mbili msimu huu.

Source: Mwanaspoti

Tupia Comments