Zoezi la kuendelea kuwatimua watendaji wasiowajibika katika ofisi za umma limeendelea kuchukua headlines kila siku..leo inawahusu wakurugenzi wa Manispaa za Kigoma, Katavi na Mpanda ambao wamesimamishwa kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene.
Uamuzi wa Mh.Simbachawene umekuja baada ya kubaini upotevu wa wa fedha za umma.
Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo Cha Mawasiliano Ofisi ya Rais imesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye Dhamana kama Sheria inavyo elekeza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Suleiman Lukanga ana kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 90 na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200.
Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Lauteri John ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Pia amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo kwani Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.