Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza Mara moja msako wa kuwakamata Watuhumiwa wa Wizi na unyang’anyi kwa kutumia silaha maarufu Kama Panya road na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia taharuki iliyoibuka Miongoni mwa Wananchi Baada ya kutokea kwa matukio ya uhalifi maeneo mbalimbali ikiwemo Tabata, Chanika, Zingiziwa na kunduchi ikihusisha vijana wa Kati ya miaka 13 Hadi 21.