TANESCO wamewaomba radhi wateja kutokana na kukosekana kwa huduma ya ununuzi wa umeme wa luku leo June 7,2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu kupitia ukurasa wa Twitter imeeleza sababu ya kukosekana kwa huduma ni hitilafu iliyobainika wakati wa maboresho yanayoendelea katika mfumo wa manunuzi ya luku.
“Huduma ya mfumo wa manunuzi ya luku inatarajiwa kurejea leo, saa 12 jioni, tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wakiendelea na maboresho,” imeeleza taarifa hiyo.
MKE WA TB JOSHUA AVUNJA UKIMYA “NAUMIA MOYONI”, MAZISHI FAMILIA INAPANGA, RAIS NIGERIA ISHARA ZAKE”