“Bara la Afrika pekee lina Mabilione 140,000 sawa na asilimia 1 ya Mabilionea wa Dunia nzima ambapo katika idadi hiyo Mabilionea 5,740 wanatoka Nchini Tanzania ambao wanamiliki asilimia 4.2 ya utajiri katika kundi la Mabilonea wa Afrika”
“Miongoni mwa Mabilionea 5,740 waliopo Tanzania, 115 sawa na asilimia mbili wana utajiri wa zaidi ya dola milioni 30 (Utra High Net Worth Individuals) na wanamiliki zaidi ya asilimia 28 ya utajiri wote wa mabilionea wa Tanzania”
“Kati ya hawa waliopo Tanzania wengi wamesajiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) na wanalipa kodi zao Idara ya Walipakodi Wakubwa na wamewekeza katika sekta za viwanda, nishati na madini, sekta ya fedha, mawasiliano na uchukuzi, utalii na makazi” ——— asema Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba Bungeni leo akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi.