Burundi na Tanzania zimetia saini mkataba wa dola milioni 900 kujenga reli itakayounganisha nchi hizi mbili jirani.
Reli hiyo ya standard gauge ya Kilomita 282 itaanzia Uvinza mkoani Kigoma hadi Gitega, mji mkuu wa kisiasa wa Burundi.
Waziri wa Mipango na Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba amesema nchi hizo mbili “zitatafuta maeneo ambayo tunaweza kupata fedha za kufadhili mradi huo”.
Inatarajiwa kuwa reli hiyo itaunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi kadhaa jirani zisizo na bandari, zikiwemo DR Congo na Rwanda.