Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 imepangiwa makundi yake ya michuano ya kufuzu huko Cairo Misri kwenye makao makuu ya shirikisho la soka Afrika CAF ambapo timu kubwa zimeonekana kupangwa kwenye nafasi za kwanza huku zikipangwa na mataifa madogo kama ulivyo utaratibu wa kugawa nafasi kuendana na viwango vya ubora.
Timu ya taifa ya Tanzania imepangwa kwenye Kundi G ambako inaambatana na timu za taifa za Misri , Nigeria na Chad na makundi mengine ni haya hapa chini.
Kundi A ; Tunisia , Togo , Liberia , Djibouti . Kundi B ; Congo Drc , Angola , CAR , Madagascar.
Kundi C Mali , Equatorial Guinea , Benin , South Sudan. Kundi D; Burkina Faso ,Uganda , Botswana , Comoros.
Kundi E; Zambia , Congo , Kenya , Guinea-Bissau. Kundi F ; Cape Verde , Morocco , Libya, Sao Tome.
Kundi G; Nigeria , Egypt , Tanzania , Chad. Kundi H; Ghana , Mozambique , Rwanda , Mauritius.
Kundi I; Ivory Coast , Sudan , Sierra Leone , Gabon . Kundi J; Algeria , Ethiopia , Lesotho , Seychelles.
Kundi K; Senegal , Niger , Namibia , Burundi . Kundi L ; Guinea , Malawi , Zimbabwe , Swaziland.
Kundi M ; Cameroon , South Africa , Gambia , Mauritania .
Michezo ya kufuzu kwa makundi haya itaanza kupigwa June 2015 mpaka mwakani na washindi wa makundi haya na timu mbili zilizomaliza hatua hii kwa rekodi bora kuliko nyingine zitaungana na wenyeji timu ya taifa ya Gabon kukamilisha timu 16 zitakazoshiriki michuano ya Afcon mwaka 2017.