Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu imeutaja wizi wa alama za barabarani kuwa ni changamoto ambayo inakwamisha utekelezaji wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara.
Akitoa taarifa katika kikao cha Bodi ya barabara kilichofanyika leo Ijumaa Julai 16, 2021 mjini Bariadi, Mratibu wa TARURA mkoa wa Simiyu, Mhandisi Myamagalula Ndango amesema wizi wa vyuma vya madaraja, makaravati, vyuma vya alama za barabarani pamoja na mchanga wa madini kando kando ya barabara ni changamoto wanazo kabiliana nazo.
Amesema mbali na changamoto hiyo pia maeneo yenye changarawe ambazo zinatumika katika ujenzi wa barabara yanamilikiwa na watu binafsi hivyo kusababisha upatikanaji hafifu wa changarawe wakati wa matengenezo.
“Wataalam wanaendelea kufanya utafiti juu ya namna ya kupata maeneo ya kuchimba changarawe ambayo yatamilikiwa na TARURA pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwa walinzi wa miundombinu ya barabara,” Mhandisi Myamagalula Ndango