Top Stories

Shigongo amuomba Rais Samia amuondoe Mkurugenzi “pesa zinaliwa”

on

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuwahamisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa pamoja na Idara ya uhasibu katika Halmashauri hiyo, akiwatuhumu kwamba wamekuwa wakiibia fedha halmashauri hiyo.

“Mimi nilikuwa sijawahi kuhitilafiana na Mkurugenzi wangu hata mara moja mpaka nilipoanza kufuatilia mapato ya ndani, mimi naomba Mheshimiwa Rais aniondolee Mkurugenzi, aniondolee idara ya uhasibu isipokuwa amuache Mwekahazina peke yake,” Mbunge Shigongo.

“Ninaomba Halmashauri ya Buchosa ikaguliwe sababu pesa zinapotea, fedha zinaliwa, mtu anakuja pale anafanya kazi miezi miwili tayari ana nyumba mbili wakati kipato chake hakitoshi kujenga nyumba mbili, kwa niaba ya watu wa Buchosa nasema jambo hili hatulikubali niungwe mkono ama nisiungwe mkono na Madiwani mimi nitasimama imara kuhakikisha fedha zinzokuja zinatumika vizuri”.

 

Soma na hizi

Tupia Comments