Unaambiwa ni ndani ya kama dakika 30 tu mtu kaajiriwa na kaikosa kazi ndani ya muda huohuo, kisa michoro ya tattoo… Claire Shepherd ni mwanamke ambaye ana umri wa miaka 27, kutoka Swansea, Wales… alifanyiwa Interview kwa njia ya simu na Kampuni ya Dee Set inayojihusisha na masuala ya Usafirishaji Uingereza, akapewa majibu kwamba amefanikiwa kupita kwenye nafasi ya kazi kwa hiyo ni mwajiriwa na Kampuni hiyo.
Baada ya dakika kadhaa, Claire alitumiwa email ambayo ilikuwa na maelekezo juu ya aina ya mavazi na mwonekano ambao anatakiwa kuwa nao akiwa kazini.
Hapo ndio lilipoanzia tatizo !! kwenye Masharti ya kazi iliandikwa kwamba kama kuna mtu ana tattoo anatakiwa kuvaa mavazi ya kuzifunika ili mtu mwingine yoyote asizione wakati akiwa kwenye mazingira ya kazi… wakati huo yeye ana michoro ya tattoo mpaka vidoleni, akaamua kuwajibu kwamba yeye ana tattoo mpaka kwenye vidole vya mikono, hapo inakuwaje?
Email ikarudi huku ikiwa na majibu ya kumkatisha tamaa zaidi, jamaa walisema kama ndio hivyo basi nafasi ya kazi kwa ajili yake haipo tena !!
Claire akapost ujumbe wa kulalamika kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu hicho alichofanyiwa na Kampuni hiyo… baada ya watu wengi kuonekana kumpa support, Kampuni ilimwita ili aendelee na kazi lakini alikataa na kusema kwamba tayari amepata kazi sehemu nyingine.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE