Mei 6 2016 ilikuwa ni zamu ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwasilisha Bungeni Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017.
Baada ya uwasilishaji huo Wabunge walipata nafasi ya kuchangia maoni yao kuhusu bajeti hiyo, hapa nakukutanisha na Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka alivyosimama na kutoa mchango wake..
>>’Mimi ninafahamu kama Mwanauchumi ni lazima viwanda vinaendana na kilimo, huwezi kuendeleza viwanda kama hujaendeleza kilimo. Ni lazima tuwe na malighafi kwamfano mazao ya mchele na alizeti‘
‘Mimi kama mchumi ntasema kwamba Taifa hili halina sababu yoyote isipokuwa katika hali ya dharura kukubali kuagiza sukari, mchele au alizeti kutoka nje, lazima kuwe na mkakati wa kulinda viwanda‘
‘Hali hiyo tujipange sasa, tulio wengi ni wakulima, wavuvi na wafugaji. Sasa mnatuwezeshaje? ninaposema sukari isiingie, ikiingia itaua viwanda vya sukari.. hata mtoto wa shule anajua hilo, lazima Wizara iwe na utaratibu wa kuingiza sukari lakini sio kutumia wafanyabiashara‘
Unaweza kuendelea kumsikiliza Profesa Tibaijuka kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA HII BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI ZAIDI YA BILIONI 81 ILIVYOWASILISHWA BUNGENI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE