1. Cristiano Ronaldo
Ronaldo alizaliwa February 5 1985 Santo Antonio Ureno jirani na miji ya Funchal na Madeira, ni mtoto wa mwisho kwa mama yake Maria Dolores do Santos Aveiro ambaye alikuwa mpishi wakati huo na baba yake Jose Dinis Aveiro ambaye alikuwa mtunza bustani za manispaa.
Jina lake la pili “Ronaldo” lilitokana na marehemu baba yake Jose Dinis Aveiro kumpenda sana rais wa 40 wa Marekani Ronald Reagan. Ronaldo anatokea familia ya kikatoliki, amewahi kukiri kutokea katika familia ya kimaskini na ilifikia wakati analala chumba kimoja yeye, kaka yake na dada zake.
Ronaldo alikuwa maarufu shuleni, alifukuzwa baada ya kumpiga na kiti mwalimu licha ya Ronaldo kukiri kuwa alikosewa heshima na mwalimu… Akiwa na umri wa miaka 14 ndipo mama yake Dolores do Santos Aveiro alipomshauri kujikita zaidi katika soka .
2. Raheem Sterling
Mtu wangu huyu, hivi karibuni jina lake limekuwa headlines katika vyombo vingi vya habari duniani kuhusiana na uhamisho wake kutoka Liverpool kwenda Man City.
Licha ya kuwa ni raia wa Uingereza kwa sasa, jamaa amezaliwa Kingston Jamaica, akiwa na umri wa miaka saba alihamia London na mama yake akaenda kusoma Copland School iliyopo Wembley kaskazini magharibi mwa London… Kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja wa kike Melody Rose aliyezaliwa 2012. Baba yake mzazi aliuawa Jamaica yeye akiwa na miaka 9 wakati huo.
3. Ronaldinho
Jamaa jina lake kamili ni Ronaldo de Assis Moreira. Dunia inamtambua na kumheshimu kwa sababu ana uwezo wa ziada wa kumiliki na kuchezea mpira anavyotaka, kwa lugha ya kimpira tunasema mpira unamtii huyu jamaa, ila uwezo wake wa kumiliki na kuchezea mpira ulianzia akiwa na umri wa miaka nane tu na ndipo alipopewa jina la “Ronaldinho” sababu alikuwa na umbo na umri mdogo lakini ana uwezo.
Alianza kuingia katika headlines ya vyombo vya habari akiwa na umri wa miaka 13 tu baada ya kufunga magoli 23 katika mechi iliyomalizika 23-0 dhidi ya timu ya huko huko kwao brazil.
Ronaldinho alianza kutambulika kama star chipukizi wa soka 1997 katika michuano ya World Cup U-17 baada ya kufunga mabao mawili kwa mkwaju wa penati mashindano yaliofanyika Misri.
Hao ndio mastar wa leo wa TBT story na picha zao.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.