Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo Aug 06 waliwaalika wanamuziki wa Tanzania kwa ajili ya semina ya namna ya kuziweka salama akaunti zao za mitandao ya Kijamii baada ya malalamiko yaliyoripotiwa na baadhi ya wasanii kuhusu matapeli namna wanavyotumia majina yao kwenye mitandao kutapeli watu.
Semina hii ya leo ilikuwa imewalenga wanamuziki mbalimbali wa Tanzania wakiwemo wa Band,Taarabu Nyimbo za Asili na wanamuziki wa Bongo Fleva,jumla yao waliopata mualiko walikuwa 70 ingawa mahudhurio yao yanakadiriwa kuwa 20.
Meneja wa Mawasiliano(TCRA) Inocent Mungi baada ya semina hiyo alipata nafasi ya kuongea na millardayo.com >>’Kiukweli wasanii wametuangusha kidogo,tulikua tunawategemea 70 ambao walialikwa,wao wamefika 20 kwa jumla ya wanamuziki wote,tuliwapa taarifa kupitia vyama vyao wengine tuliwafahamu na wapo waliomba wenyewe,katika watu ambao hawajaja 17 walisema wangekuja na hawakutokea’
‘Tuliona tuanze na Wanamuziki kwa mwaka huu wa kwanza wa fedha kwa sababu ndiyo walioathirika zaidi wanatumika vibaya sana kwenye kueneza maneno mabaya wengine majina yao yanatumika kwenye utapeli tulitaka kuwaelimisha hapa namna ya kuokoa akaunti zao ambazo zimevamiwa na jinsi ya kujiweka vizuri lakini wale waliofika tunategemea watawatumia kutoa Elimu’.
Upande wa Bongo Fleva wasanii ambao mpaka mwisho walioonekana ni Vanessa Mdee(Vee Money),G Nako,Nikki wa Pili na Dabo.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos