Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imekamilisha awamu ya kwanza ya udahili kwa waliomaliza kidato cha sita na wenye vyeti vya nje ya nchi.
Jumla ya waombaji waliosajiliwa ilikuwa 55,347 na waombaji wenye sifa waliopata nafasi ya chuo jumla ni 30,731 na waombaji ambao hawajapata nafasi ya chuo jumla ni 24616. Waombaji wengi wamekosa nafasi katika vyuo sababu kubwa ikiwa ni ushindani uliopo kutokana na uhaba wa nafasi katika kozi hizo.
TCU imeongeza muda wa udahili kuanzia September 12 hadi 23 2016 kwa waombaji wenye sifa ili wapate kuchagua kozi zenye nafasi.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
NI KWELI UCHUMI WA NCHI UMESHUKA ? SERIKALI IMELIJIBU HILO KWENYE VIDEO HII