Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii ya kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘TCU YATOA SIFA MPYA KUJIUNGA VYUO VIKUU’
#MTANZANIA TCU yatangaza utaratibu mpya wanaochukua shahada huku wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa pic.twitter.com/blP5ROP2cj
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
Gazeti hilo limeandika kuwa Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU‘ imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi ka kukosa sifa na vigezo.
Utaratibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Sifa hizo zilizowekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana, Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa ‘D mbili’ pointi 4.0. Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokan na ufaulu wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.
Taarifa hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 ili wawe na sifa za kudahiliwa z, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa ‘C mbili’ pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B+=4; B=3; C=2; D=1.
Kupitia tovuti hiyo iliyoonyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu watahitajika kuwa na ufaulu wa alama ‘D mbili’ 4.0 kupitia mchanganuo wa A=5; B=4; C=3; D=2; E=1.
Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F=0-38.
Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na baraza ka Taifa la mitihanai ‘NECTA’ na mafunzo ya ufundi ‘VETA’
Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.
Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udaahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA.
SOURCE: Gazeti la Mtanzania
Unaweza kuzipitia habari nyingine hapa chini kwenye magazeti ya leo
#NIPASHE Ukata unavyotesa madada poa Dar, walia awamu ya tano kukimbiza wateja, washusha bei hadi 'buku' pic.twitter.com/BTstxbsICF
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#NIPASHE Mrema afurahia uteuzi wa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Taifa ya Parole asema Rais Magufuli amelipa ahadi yake pic.twitter.com/Dy0yjeqyiy
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#NIPASHE Matokeo ya kidato cha sita yanayoonyesha shule nyingi za Z'bar zikiburuta mkia yamewasononesha wengi pic.twitter.com/0S9SVJrkFu
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI NECTA yatumia mfumo mpya kupanga matokeo kidato cha sita ili kuongeza thamani ya madaraja ya watahiniwa pic.twitter.com/0Ke3A6rtRD
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI RC Tanga amewataka wananchi mkoani humo kuishi kwa amani kwa kuwa sasa hakuna tena tishio la ugaidi pic.twitter.com/IVpe0nWsl4
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI Onesmo Ole Nangole amekata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge jimbo la Longido pic.twitter.com/4RHDYsSTCX
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI Jaji Mkuu, Othman Chande amesema mahakama ya mafisadi itakuwa na masijala kila kanda pic.twitter.com/41EPu0kArZ
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kuwa 11% ya watanzania nchini wamejiandikisha na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa pic.twitter.com/8w2FvhzHP3
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MWANANCHI Waziri mkuu, Majaliwa amefungua duka la sita la bohari kuu ya dawa 'MSD' hospitali ya wilaya ya Ruangwa pic.twitter.com/MjwMIT2U9g
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#JamboLEO Wadau wa elimu wataja sababu kushuka kwa ufaulu kidato cha sita ikiwemo mapenzi ktk shule za mchanganyiko pic.twitter.com/46xnl1tfeJ
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MTANZANIA TCU yatangaza utaratibu mpya wanaochukua shahada huku wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa pic.twitter.com/blP5ROP2cj
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MTANZANIA Watoto wanane waliozaliwa na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi hufanyiwa upasuaji kila wiki MOI pic.twitter.com/PYKIVsaqEX
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#MTANZANIA Wanafunzi elimu ya juu waipa saa 72 serikali kuwapatia fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo pic.twitter.com/07w0qXwAaN
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
#HabariLEO Prof Mkumbo apendekeza serikali kuachana na ada elekezi badala yake itoze kodi shule binafsi pic.twitter.com/jBnzixbaEi
— millardayo (@millardayo) July 17, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 17 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI