Top Stories

Kiongozi wa Upinzani ashtakiwa kwa Uhaini

on

Kutoka nchini Ghana, Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha Upinzani nchini humo National Democratic Congress (NDC) amefunguliwa kesi ya uhaini kutokana na alichokiongea kwenye moja ya kituo cha radio nchini humo.

Koku Anyidoho alikamatwa katika mkutano wa waandishi wa habari huko Accra Jumanne March 27, 2018 ambao uliandaliwa na kundi la vyama vya upinzani kupinga makubaliano ya ushirikiano wa utetezi kati ya Ghana na Marekani.

Kukamatwa kwake kulisababisha vurugu kubwa iliyofanywa na wafuasi wa chama hicho ambao walifanya vurugu hizo kwenye Makao Makuu ya Polisi kwenye Mji Mkuu Accra, wakishinikiza aachiwe huru.

Lowassa, Sumaye, Wafuasi wa CHADEMA walivyojitokeza nje ya Mahakama

 

Soma na hizi

Tupia Comments