Ukimwambia mtu yoyote kwamba unatafuta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yako, moja kwa moja mawazo ya watu wengi ni kwamba nyumba yako inahitaji mawe, mchanga, cement na vitu vingine kama hivyo… lakini moja ya stori ambazo millardayo.com huwa inakuwekea ni story zenye vitu tofauti na ilivyozoeleka.
Ukiachana na story ya nyumba iliyotengezwa kwa Makontena, nyumba za mbao na vioo, uko na huu ubunifu ambao kiukweli ni wa kuvutia sana ambao Jono Williams amebuni toka New Zealand, Mjengo wake kaupa jina la Skysphere na imemchukua miaka mitatu tu mpaka kila kitu kukamilika.
Hizi pichaz ni hatua za kwanza kwenye ujenzi wenyewe.
Mambo yakaendelea vizuri, ujenzi unasogea tu kwenye hatua ya kukamilika.
Ujenzi umefikia pazuri, Time ya kuona na vitu vya ndani mtu wangu.
Kwanza kabisa hii nyumba kila kitu kimeunganishwa na system ya App ambayo mwenye nyumba yuko nayo kwenye simu yake, unaambiwa hata kama vinywaji vimepungua kwenye fridge hana haja ya kufunua kuangalia, App ya kwenye simu yake inampa majibu yote.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE