Mabingwa wapya wa Michuano ya kombe la mataifa ya Africa Afcon Timu ya taifa ya Ivory Coast wamezawadiwa kitita cha fedha taslimu dola za kimarekani Milioni 3.4 ikiwa ni zawadi ya kutwaa ubingwa huo ambao mara ya mwisho waliutwaa mwaka 1992 .
Zawadi hiyo imemjumuisha kocha Herve Renard ambaye alipewa fedha taslimu dola 129,000 ikiwa ni zawadi yake baada ya kuiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa huu .
Ukiachilia mbali fedha taslimu , wachezaji wa timu hii kila mmoja amekabidhiwa zawadi ya nyumba yenye thamani ya dola 52,000/= ambayo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya milioni 70 huku pia wakipewa kiasi hicho cha fedha kama zawadi ya kuwa mabingwa .
Chama cha soka cha Ivory Coast kwa upande wake kimepewa fedha taslimu dola 429,000/= huku watu wote walioko kwenye bechi la ufundi wakipewa kitita cha fedha dola laki 520,000/= ambazo wamegawana .
Jumla ya fedha hizi ambazo zimetolewa na rais wa taifa hili Alassane Outtarra ni dola milioni 3.4 ambazo zimekuja kama zawadi ya kuliletea taifa heshima kubwa kwa kutwaa ubingwa wa michuano ya mwaka huu .
Rais Alassane Outarra amewashukuru wachezaji wa timu hii kwa heshima kubwa waliyoiletea nchi yao na amewatunukia tuzo ya juu ya taifa hili ukiachilia mbali fedha taslimu ambazo kila mchezaji amepata .